Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua dereva bodaboda

HomeKitaifa

Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua dereva bodaboda

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kanda ya Mbeya imemhukumu Emmanuel Msomba kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mauaji ya dereva bodaboda, Isack Kazuka kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.

Shauri hilo lilisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mkoa wa Mbeya, Zawadi Laizer na kusema kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ulithibitisha kabisa kuwa Emmanuel alitenda tukio hilo.

  > Bodaboda walalamika kuchapwa bakora na polisi

Katika ushahidi uliotolewa mahakamani unaeleza kuwa Isack alikuwa akisafiri na bodaboda kutoka Mji wa Tunduma kwenda Sumbawanga alipofika njiani Emmanuel alimuomba lifti na Isack alimkubali lakini baada ya mwendo kidogo katika safari yao bodaboda iliharibika ikabidi Isack ashuke aitengeneze, ndipo Emmanuel akampiga na kitu kizito kichwani kisha akampora simu na fedha.

Emmanuel alipata nafasi ya kujitetea ambapo katika utetezi wake alisema yeye aliomba tu lifti kwa Isack na waliachana naye kwa fundi alikokuwa anatengeneza pikipiki hiyo baada ya kuharibika wakiwa safarini.

> “Utafiti: Bodaboda inavyoweza kuharibu iPhone yako”

Wakili aliyekuwa anawakilisha upande wa Jamhuri, Davice Msanga aliomba mahakama kutoa adhabau kama sheria inavyoelekeza kutokana na watu wengi kukatisha maisha ya wenzao kwa sababu ya tamaa za fedha na mali.

error: Content is protected !!