Binti wa Mayweather hatarini kufungwa miaka 20 kwa kugombea penzi

HomeKimataifa

Binti wa Mayweather hatarini kufungwa miaka 20 kwa kugombea penzi

Aprili 2, 2020 Yaya Mayweather alikwenda nyumbani kwa mpenzi wake, rapa NBA YoungBoy na kumkuta aliyewahi kuwa mpenzi wa mchumba wake huyo, Lapattra Lashai Jacobs, na kumwambia Lapattra aondoke hapo nyumbani kwani NBA Youngboy ni mchumba wake.

Baada ya kuzozana sana walifikishana hadi jikoni ambapo binti huyo wa Floyd alichukua visu viwili, pale Lapattra alipozidisha hatua tu, Yaya alimchoma kisu kimoja na baadaye kumshindilia tena kisu cha pili.

Yaya huenda akahukumiwa kifungo cha hadi miaka 20 jela kwa kosa la kumchoma kisu mara mbili mzazi mwenza wa mchumba wake, NBA Youngboy.

Kwa sasa Yaya anakabiliwa na kosa la kumshambulia mtu na silaha hatari huku akisubiri hukumu yake ambayo itasomwa mapema mwezi Februari 2022.

error: Content is protected !!