Fahamu vyakula aina 7 hatarishi kwa malezi ya mtoto wa umri chini ya mwaka 1

HomeElimu

Fahamu vyakula aina 7 hatarishi kwa malezi ya mtoto wa umri chini ya mwaka 1

Katika malezi na ukuaji mtoto aliye chini ya mwaka mmoja huwa na masharti mno katika aina ya vyakula. Ni vizuri ukajua ni vyakula gani ambavyo mtoto hastahili kulishwa kutokana na umri wake.

Leo tumekuandalia baadhi ya vyakula kama ifuatavyo:

Soya
Soya huchangia kutengeneza mzio (allergy), ambapo husabaisha kupoteza vitamini kwenye mwili wa mtoto hivyo ni vizuri wapewe wakiwa na umri zaidi ya mwaka mmoja na kuendelea.

Sukari
Kiwango kikubwa cha sukari si kizuri kwa watoto kwani huaribu meno na fizi za mtoto huwa katika hatua za kuotesha meno hivyo iwapo atapewa sukari anaweza kuharibu ukuaji wake au mtoto kupata matatizo ya kisukari baadaye. Mbadala wake kwenye uji unaweza kutumia ndizi mbivu ambayo ina sukari ya kutosha kwa kutumia kwa chakula cha mtoto, saga ndizi mbivu halafu changanya kwenye uji ulioiva ili kupata sukari asilia.

Asali
Kwa kawaida inatabia ya kubeba bakteria ambao baadaye humwathiri mtoto aliyechini ya miezi 12. Kwa mtoto mwenye umri wa kuanzia mwaka mmoja na kuendelea hawawezi kumwathiri kwa kuwa mwili wake unakinga ya kupigana nao.

  > Vyakula Kumi (10) vinavyoongeza hamu ya tendo la ndoa

Chumvi
Kuna tabia imejengeka kwa baadhi ya wazazi wanadhani chakula kisipokuwa na chumvi mtoto hawezi kula, dhana hii ni ya uongo kabisa. Kipindi hiki ndio mtoto anaanza kujifunza kula hivyo hajui ladha yoyote kuwe na chumvi au la! Chumvi ina madini ya sodium ambayo yanaweza kwenda kuathiri figo au kuathiri moyo na kupata matatizo ya shinikizo la damu. Hivyo, haihitajiki chakula kiwe na chumvi hata kama ukitumia basi iwe kiwango kidogo sana.

Samaki
Samaki wenye madini ya zebaki (mercury) kwa wingi, kwa mfano papa, chuchunge, dagaa wakubwa na wengineo. Samaki hawa wana tabia ya kuathiri mfumo wa neva. Badala yake mpe sangara, sato au salmon, hawa wana mafuta ya kutosha na omega 3 zitakazo msaidia kukuza ubongo na kumfanya kuwa na akili.

Korosho
Vitu kama karanga au korosho, mtoto asipewe kutafuna vinaweza kumkwama kooni. Kama ni karanga basi iwe ni ya kusagwa na wapewe watoto kuanzia miezi sita.

Mafuta ya kupikia
Mtoto hahitaji mafuta kwenye chakula chake kwa kuwa vyakula anavyopikiwa vinamafuta ya asilia kama nyama, kuku, samaki iwapo utatumia mafuta, basi ni vema ukatumia ‘butter’ isiyo na chumvi au olive oil. Haya ni mafuta sahihi ambayo hayana madhara kama mafuta mengine na yatamsaidia kwenye ukuaji wake.

error: Content is protected !!