Diamond: Mimi ndio chanzo tuzo kufa

HomeBurudani

Diamond: Mimi ndio chanzo tuzo kufa

Mmiliki wa lebo ya Wasafi na msanii, Diamond Platnumz amefungua na kueleza kuwa yeye ndiyo chanzo cha kusitishwa kwa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) miaka ya nyuma kwa kusema mashabiki walikasirika yeye kunyimwa tuzo na kushindwa kuibuka mshindi katika baadhi ya vipengele.

“Tuzo za Tanzania sababu ya kufa ni mimi, mimi nilinyimwa tuzo wakapewa watu wengine ambao mimi nilikua nastahili, wadhamini wakamind(kukasirika), walijitoa yani yalitokea mambo mengi sana,

“Sababu ya tuzo kufa i was the reason, kwa sababu mimi nilinyimwa watu wakamind, Watanzania wakazungumza. So ili zinapokuja mpya naziamini vipi? Lazima nizitazame kwanza nione zina uhalisia na ukweli au zina uongo ndani yake,” alisema Diamond.

Akizungumza kwenye mahojiano na mtangazaji Salim Kikeke wa BBC Swahili, Diamond pia aliweka wazi suala lake la kutaka kuoa hivi karibu na pia kulaani kitendo cha baadhi ya watu kutangaza kwamba anapangiwa maamuzi ya ndoa na mama yake mzazi.

error: Content is protected !!