Msimamizi wa uchaguzi Kenya atoweka

HomeKimataifa

Msimamizi wa uchaguzi Kenya atoweka

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya, Wafula Chebukati amevitaka vyombo vya usalama kusaidia kumrudisha afisa wa IEBC ambaye alitoweka tangu Agosti 11.

Daniel Mbolu Musyoka, afisa msimamizi wa eneo bunge la Embakasi Mashariki mwenye umri wa miaka 50 alitoweka katika mazingira ya kutatanisha siku ya Alhamisi, mwendo wa saa tatu asubuhi. Familia na Tume zimejaribu kuwasiliana bila mafanikio.

Kisa hicho, hata hivyo kimeripotiwa polisi ambao walianzisha msako wa kumtafuta afisa huyo. Kulingana na polisi, tukio hilo liliripotiwa na APC Dennis Maina Gichure, mlinzi wa Musyoka kwamba alimsindikiza kutoka nyumbani kwake katika Shule ya Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki hadi kituo cha kujumlisha kura ndani ya eneo hilo.

“Mnamo saa 3:45 asubuhi, alipokea simu lakini hakurudi hadi sasa. Simu yake ya mkononi ilikuwa imezimwa. Kazi zake katika kituo cha kujumlisha kura zinasimamiwa na msimamizi msaidizi,” Mwenyekiti wa Tume alisema Ijumaa. Kulingana na wapelelezi hao, Musyoka hakuwa mgonjwa lakini alikuwa na historia ya kuwa na sukari nyingi kwenye damu.

“Msako umefanywa katika hospitali kadhaa zinazozunguka, lakini bado hajafuatiliwa. Msako bado unaendelea. Ripoti ya maendeleo itafuata,” polisi walisema.

error: Content is protected !!