Zifahamu rekodi 6 za Manchester United zilizovunjwa na Liverpool ligi kuu ya England

HomeMichezo

Zifahamu rekodi 6 za Manchester United zilizovunjwa na Liverpool ligi kuu ya England

Kufuatia klabu ya Manchester United kupoteza mchezo wao Jumapili dhidi ya mahasimu wao wakubwa Liverpool, kwa kichapo cha goli 5-0, Liverpool imevunja rekodi kadhaa za Manchester United iliyojiwekea ndani ya ligi kuu ya England.

Zifuatazo ni rekodi zilizovunjwa na Liverpool dhidi ya Manchester United:

  1. Hii ni mara ya kwanza katika Historia ya Man United ndani ya EPL kuongozwa kwa magoli 4-0 kipindi cha kwanza (First half)
  2. Mo Salah ameweka Rekodi ya kufunga katika Michezo 10 mfululizo akiwa Liverpool.
  3. Klopp anaweka Rekodi ya kuwa Kocha pekee wa Liverpool ambaye hajapoteza mchezo hata moja kati ya michezo 7 mfululizo dhidi ya Man United ‘katika PL’.
  4. Vipigo vitatu vikubwa alivyofungwa Man United karibuni vyote amepigwa Mwezi wa 10, (6-1 vs Spurs Oktoba 2020) na (6-1 vs Man City Oktoba, 2011).
  5. Rasmi sasa Mo Salah ndiye Mwafrika aliyefunga magoli mengi Premier League (107).
  6. Mo Salah anakuwa Mchezaji pekee wa Kigeni (kutoka Afrika) kuifunga Man Utd katika uwanja wake wa nyumbani, Old Trafford tangu January 1992.
error: Content is protected !!