Rais Samia: Hayajamkuta nduguyo

HomeKitaifa

Rais Samia: Hayajamkuta nduguyo

Rais Samia Suluhu Hassan amewaasa waandishi wa habari pamoja na wananchi kuitumia vyema mitandao ya kijamii kwa kuzingatia aina ya maudhui wanayorusha kwenye mitandao hiyo.

Akizungumza jijini Arusha wakati wa hafla ya Siku ya Vyombo vya Habari Duniani iliyoadhimishwa mkoani humo, Rais Samia amewataka wale wanaotuma maudhui maovu kuwachafua wengine, kujiweka kwenye hizo nafasi au watu wao wa karibu.

“Mitandao ya kijamii, watoto wa Kitanzania wanajipiga picha za utupu wanaweka, ajali inatokea fresh fresh zinapigwa picha zinawekwa huko, hivi unamwekea nani atazame, hivi ukute dada yako kakaa hivyo alivyokaa anajianika huko, utajisikiaje?

“Hatuwezi kukataa kuwa mitandao ya kijamii imekuwa ni sekta muhimu ya maisha yetu. Mitandao hii inatupa fursa ya kutumia uhuru wetu kujieleza jinsi tunavyoweza… kupeana moyo katika mambo mbalimbali, kukubaliana au kutokubaliana na mambo yanayopangwa au kutekelezwa na serikali zetu au hata kumsifia mtu, kumjenga au kumharibia sifa kwenye jamii,” amesisitiza Rais Samia.

Amewataka waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele kulinda mila na desturi za Tanzania ili zisipotee na si tu kukopa kila kitu kutoka nchi za watu na kuwa wazalendo katika kukamilisha majukumu yao.

“Wale wakubwa wanaandika [habari] za kwetu kwa kina lakini na vijichumvi kidogo, lakini habari zile wanapewa na ninyi ambao wengine mnajiita mawakala wa vyombo vile. Lakini yule kule hajivui yeye akakupa wewe, atakupa kile unachopaswa kukisikia, mengine usiyopaswa kusikia hakupi, lakini sisi tunajivua wazima wazima tunapeleka,” Rais Samia akielezea tofauti ya uandishi wa habari wa nchi zilizoendelea na zinazoendelea.

Rais ameeleza kushangazwa na maneno ya Watanzania wanayorusha mitandaoni mara baada ya kujua kuwa Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amepata maambukizi ya UVIKO.

“Nimeona mitandaoni Rais wenu kaenda kuonana na Makamu wa Rais wa Marekani baada ya wiki anaambiwa yule Bibi ana Covid mimi mzima, Mtanzania kaweka kikatuni mimi ndiyo nimempa covid, ulizeni mnajiandikia tu, mie nina ngozi ngumu andikeni.”

error: Content is protected !!