IGP atuma salamu kwa wezi wa pikipiki

HomeKitaifa

IGP atuma salamu kwa wezi wa pikipiki

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka wezi wa pikipiki wilayani Arumeru mkoani Arusha kuacha mara moja tabia na kuwa hawatofurahia maamuzi yake.

Akizungumza na wananchi wa Arumeru, Kamanda Sirro amesisitiza si sawa kuona mtu anatumia milioni 2.2 kununua pikipiki alafu mwingine anaichukua kimabavu.

“Wale wanaofanya wizi wa pikipiki waache, maana mimi huwa nikifika sehemu nikatoa salamu majibu yake huwa si mazuri,” alisisitiza IGP Sirro.

Ameongeza kuwa atatuma kikosi maalum wilayani hapo kwenda kufanyia kazi tatizo hilo na kukamata wahalifu wote wa wizi wa pikipiki.

Amehimiza wananchi kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi hadi hapo askari wengine 4,000 watapomaliza masomo na kuongeza nguvu kwenye maeneo mbalimbali.

error: Content is protected !!