Aliyeimba ‘Ekwueme’ afariki dunia

HomeBurudani

Aliyeimba ‘Ekwueme’ afariki dunia

Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili kutoka Nigeria aitwaye Sis Osinachi Nwachukwu maarufu kwa wimbo wake “Ekwueme” amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 42.

Osinachi ambaye ameacha watoto wanne alifariki dunia jioni (April 8, 2022) hii baada ya kupambana na ugonjwa usiojulikana kwa takriban miezi miwili huku vyanzo vingine vikidai ni kansa ya koo.

Baadhi yake nyimbo ni pamoja na “Nara Ekele”  akiwa na Mchungaji Paul Enenche (Dunamis,Abuja), “Ekwueme”  akiwa na Prospa Ochimana na nyinginezo.

Wimbo wa Ekwueme umejipatia umaarufu sana kutokana maudhui yake huku ukitasambaa na kuimbwa na jamii kubwa duniani.

error: Content is protected !!