Mwanamke katu hatokufanyia mambo haya kama anakupenda

HomeElimu

Mwanamke katu hatokufanyia mambo haya kama anakupenda

1: Kukushuku
Kama kweli Bi. Dada anakupenda, katu hatoona tatizo la wewe kuketi na kufurahi na rafiki zako. Anachopaswa kujua ni kwamba mwanaume anaweza kuchagua rafiki na anaweza kujiongoza na pia, na mwanaume anaweza kuwa na muda na watu wengine muda mwingine na huenda alishakuwa na marafiki kabla ya kukutana na wewe. Mapenzi ni muhimu sana, lakini marafiki wa kweli nao hutujenga tuwe bora katika maisha yetu ya kila siku. Wanaume huu usiwe uchochoro wa kurutubisha maovu kuona mwanamke wako hakunji sura akuonapo na rafikizo, bali ni wakati wa kutompa mashaka juu yako, kuwa muwazi, atambue rafiki zako na uwe huru muda wote ili mwanamke asipande mbegu ya mashaka juu yako.

2: Kukuvunjia heshima
Mwanaume hutokaukwa na koo kuomba au kusisitiza heshima kila mara. Mwanamke anayekuhusudu kweli basi heshima kutoka kwake si kitu cha kulazimisha. Sasa hapa kuna woga na heshima, wapo wanawake wanawaogopa sana wenza wao kutokana na manyanyaso wanayopitia kutoka kwao. Kimsingi mwanamke anapaswa akuheshimu na wewe umheshimu, yaani muheshimiane. Heshima ni kitu cha bure walishasema wahenga, kama ukiona unaingia gharama hata kama sio ya fedha kwenye kudai heshima, ujue upendo umeshaota mbawa ndani ya makazi yako.

3: Usaliti
Uzuri wa wanawake ni kwamba kwao hisia zinaanza halafu upendo hufuata, wanaume huanza kutamani kwanza halafu hupenda baada ya muda kidogo. Mwanamke kama kweli anampenda mtu, na mtu yule anafanya inayompasa kufanya kwa mwanamke huyo, basi abadani mwanamke huyo hatodiriki kufanya tendo na mwanaume mwingine. Hata ikitokea mwanaume amesafiri, bado mwanamke atasubiri na atajichunga kwa ajili ya mwanaume.

4: Kutokukuonea huruma
Huruma ni vaza la asili la wanawake wote naweza kusema hivyo. Lakini kuna huruma ya mwanamke kwa mwanaume wake. Huruma hii utaiona kama mazingira yafuatayo, kutokana na kazi mwanaume anazofanya mwanamke atakutafuta au kutuma text kutoa pole. Huruma pale unatoa hela na kumpatia lazima ataji mfuko wako, ndugu zako au hata mahitaji yako kabla hajapokea. Huruma hii ukiipata kaka ujue umemjaa mwanamke huyo kwenye moyo wake.

error: Content is protected !!