Ufilipino yasogeza mbele umri wa kuanza mapenzi

HomeKimataifa

Ufilipino yasogeza mbele umri wa kuanza mapenzi

 

Nchi ya Ufilipino imekubali kuongeza umri wa wananchi kuridhia kufanya mapenzi kutoka miaka 12 baada ya vita kali kutoka kwa wanaharakati za haki za wanawake na watoto.

Sheria hiyo inayomruhusu mtu mwenye miaka kuanzia 12 kufanya mapenzi iliwekwa mwaka 1997 nchini humo ikiwa ni umri mdogo zaidi duniani na hadi sasa imeonekana kuchochea zaidi vitendo vya ubakaji unyanyasaji wa kijinsia.

Desemba 2020 wimbi la kubadili sheria hiyo lilishika hatamu hadi lilipofanikiwa majuzi Machi, 2022 na Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino kusaini kuongeza umri huo hadi miaka 16.

Huku nchi nyingi za Afrika zikiweka umri wa miaka 18 kama umri wa mtu kuweza kufanya maamuzi sahihi kuhusu maswala mengi yahusuyo maisha yake,
Sudan ndiyo nchi ya Africa yenye umri mdogo zaidi kisheria wa ruksa ya kufanya mapenzi kwa umri wa miaka 13.

Cameroon na Niger ikiweka miaka 21 kama umri halali kisheria kwa mtu kufanya mapenzi.

Nini maoni yako kuhusu jambo hili?

error: Content is protected !!