Kamwe usimfanyie mwanaume mambo haya matatu

HomeElimu

Kamwe usimfanyie mwanaume mambo haya matatu

Katika mahusiano kuna vitu ambavyo hautakiwi kabisa kumfanyia au kumwambia Mwanaume wako. Haijalishi urafiki au ukaribu mlionao lakini kamwe usithubutu kufanya mambo haya:

1.Muda na umakini
Epuka kumuomba mwanaume atenge muda kwa ajili yako na kukupa umakini kwani kumwambia hivi kutamfanya asione umuhimu wako. Yeye kama Mwanaume anapaswa kutenga muda na kukupa umakini kama kweli anakupenda na kukuthamini mpenzi wake.

2.Mapenzi na heshima
Kama kweli anakupenda basi atakuheshimu na kuonesha upendo huo kwako. Usitumie nguvu kulazimisha akupende na kukuheshimu kwani hilo ni jukumu lake na endapo atashindwa kufanya hivyo basi ni heri ukaendelea na maisha yako.

3. Usimuombe awe na wewe.
Kamwe usije ukamuomba awe na wewe katika maisha yako. Kufanya hivyo kunaonesha wazi kwamba mtu huyo havutiwi na wewe na ndio maana unamlazimisha awe nawe.Kumbuka, usiruhusu mtu akawa kipaumbele kwenye maisha yako na wewe kuwa chaguo, siku zote penda maisha yako na zingatia umuhimu wa furaha yako kwanza.

error: Content is protected !!