Ujumbe wa Samia Kwa Polepole

HomeKitaifa

Ujumbe wa Samia Kwa Polepole

Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaapisha viongozi wawili kati ya tano aliowateua jana Machi 15 ambao ni Bw. Humphrey Polepole na Bw. Waziri Kidamba leo Machi 16 kwenye viwanja vya Ikulu, Chamwino, Dodoma.

Mhe. Samia Suluhu amemteua Bwana Waziri Kindamba Waziri kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Bwana Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Mwita Rubirya ambaye amestaafu kwa umri pia amewateua Bwana Humphrey Hezron Polepole kuwa Balozi wa Tanzania Nchi ya Jamhuri ya Malawi.

“Mheshimiwa Balozi najua baada ya hapa watakuweka darasani kwanza pale Chuo ch Diplomasia utakapotoka pale kabla hujaenda Malawi nitakutana nawe kwahiyo tutazungumza kwa urefu,”

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa unakwenda Njombe Waziri Mkuu alishasema yote, anayeondoka ,anayestaafu amefanya kazi nzuri naomba anzia hapo ongeza jitihada nenda mbele,” alisema Rais Samia Suluhu.

Aidha, Rais Samia aliwasisitiza viongozi kuhamasisha wananchi kwenda kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona pamoja na Omicron ambacho kimeibuka hivi karibuni barani Asia.

error: Content is protected !!