Kenya na Tanzania zaondoa vikwazo 56 vya kibiashara

HomeKimataifa

Kenya na Tanzania zaondoa vikwazo 56 vya kibiashara

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wamejidhatiti kuhakikisha wanaviondoa vikwazo 64 kwa sasa vinavyozuia urahisi wa kibiashara kati ya raia wa nchi hizi mbili.

Mkutano wa saba wa mawaziri unaoshughulikia sekta ya biashara ulikutana Zanzibar na kukubaliana kuondoa kero 10. Sita za Tanzania na nne za Kenya.

Kati ya hoja zilizoihusu Tanzania ni pamoja na uchelewashwaji wa vibali vya kuingiza bidhaa za maziwa zinazotoka Tanzania na adha za upatikanaji vibali kwa Watanzania kufanya kazi Kenya.

Kwa upande wa Kenya pametatuliwa kero ya uhuru wa wahandisi wa Kenya kufanya kazi Tanzania na ushirikiano wa mashirika ya ndege ya Kenya na Tanzania.

Uondolewaji wa vikwanzo 46 vya kibiashara ulisaidia kukuza biashara hadi shilingi trilioni 1.1 kutoka shilingi bilioni 885. Uondolewajiwa vikwazo 10 kutaongeza chachu huku vikwazo nane vilivyobaki vikirudisha nyuma lengo hadi hapo vitakapotatuliwa.

error: Content is protected !!