Matumaini ya DRC kujiunga EAC yaongezeka

HomeKimataifa

Matumaini ya DRC kujiunga EAC yaongezeka

 

Maombi ya DRC kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo yalitumaa kwa mara ya kwanza mwaka 2019, yapo katika hatua nzuri.Baraza la Mawaziri la EAC pamoja na kitengo cha sera wanatarajia kukutana mwishoni mwa mwezi huu kuangalia vigezo vya maombi.

Vyanzo vya karibu na sekretarieti ya jumuiya vinaeleza kuwa maombi hayo yatafanyiwa uchunguzi wa hali ya juu kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa.

Baada ya hapo maombi hayo yatapelekwa hatua ya mbele zaidi ambapo ni kwenye kikao cha marais wa nchi wanachama wa jumuiya ambao ndio wenye mamlaka ya kupitisha mwanachama mpya.

Moja ya vigezo cha uanachama wa EAC ni rekodi nzuri ya haki za binadamu, uongozi wa haki na sheria na ukaribu/ujirani kwa kupakana mipaka.

error: Content is protected !!