Zanzibar: Ajikata korodani na kuzitumbukiza chooni

HomeKitaifa

Zanzibar: Ajikata korodani na kuzitumbukiza chooni

Mbarouk Abdalla mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa Fuoni Wilaya ya Magharibi B, Unguja amejikata sehemu zake za siri na kuondoa korodani moja na kuitumbukiza kwenye shimo la choo kwa madai kuwa inampa maumivu. Kijana huyo anasadikiwa kuwa na matatizo ya akili aliyoyapata baada ya kupigwa mapanga na watu wasiojulikana miaka minne iliopita kabla ya kutokea kwa tukio hilo.

Dk. Hassan Makame kutoka hospitali ya Mnazi mmoja anasema kuwa kwa sasa kijana huyo anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu, lakini aliwataka wazazi na walezi kuwa karibu na watu kjama hao ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza hasa ukizingatia kuwa mgonjwa huyo alikua anaishi peke yake kutokana na matatizo ya akili.

Mbarouk anasema “Baada ya kutoa sehemu hiyo nilipata nafuu ila kilichonidhuru kupoteza damu nyingi na ndipo nilipokimbizwa hospitali kupatiwa matibabu” alisema Mbarouk.

error: Content is protected !!