Jinsi ya kumfundisha mtoto kuchukua tahadhari ya Uviko-19

HomeUncategorized

Jinsi ya kumfundisha mtoto kuchukua tahadhari ya Uviko-19

Mtu mzima anauwezo mkubwa wa kuelewa maelekezo kwa haraka, mfano ukimuwekea ndoo ya maji ya kunawa na sabni atajua kuwa anatakiwa kunawa na ukimpatia barakoa atajua ni ya kuvaa, lakini kwa watoto hasa wale wa ngazi ya chekechea na kwenda chini ambao bado hawama utambuzi mkubwa ya mambo yanayoendelea ni ngumu kwa wao kuelewa ni nini wafanye ili waweze kuwa salama.

Hivyo basi zifuatazo ni njia rahisi zakumwelewesha mtoto juu ya ugonjwa wa Corona (Uviko-19):

Tumia midoli kumfunza njia za kuchukua tahadhari mfano kupiga chafya na kukohoa huku amejifunika na kiwiko.
Mwambie faida za kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ikiwa ni sehemu ya tabia njema na usafi.
– Tumia nyimbo zinazoimbwa kwa vitendo, mfano kunawa mikono kwa maji safi na sabuni na kutumia vitakasa mikono.
– Mnunulie vifaa vya usafi ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya watoto ili kumpa hamasa ya kuvitumia.
– Mjibu kwa mifano na ufasaha maswali yote kuhusu ugonjwa huona kama hauna taarifa sahihi usimjibu mpaka utakapozipata.
– Watoto ndio taifa la kesho, hivyo ni wajibu wetu kuwalinda na kuhakikisha wanakua salama ili kuweza kuwasaidia kufikisha malengo na kutimiza ndoto zao.

error: Content is protected !!