Abakwa na wasichana wawili, hoi hospitali akipigania maisha yake.

HomeKimataifa

Abakwa na wasichana wawili, hoi hospitali akipigania maisha yake.

Mwanaume mmoja nchini Zimbabwe mwenye umri wa miaka 27 anapigania maisha yake kwa sasa hospitalini baada ya kubakwa na wanawake wawili. Polisi nchini Zimbambwe wamesema kuwa mwanaume huyo limemsibu tukio hilo wakati anakwenda kwa shangazi yake kumchukua mke wake, akiwa njiani akielekea huko alipanda taxi ambayo ilikuwa na wanawake wawili na mwanaume mmoja ndani.

Wakati gari inaenda ghafla ilibadili ruti na kuelekea sehemu nyingine, aliuliza kijana aliyebakwa na alijibiwa kuwa wanakwenda kumshusha abiria mmoja. Punde gari ilisimamishwa kwenye mazingira yenye kificho, kijana aliyebakwa alihisi hatari na kutaka kukimbia, mwanaume aliyekuwamo kwenye gari alimvuta na kumdunga sindano yenye dawa za kulevya na kijana huyo kupoteza fahamu.

Baada ya hapo wasichana hao walitimiza haja zao kwa mwanaume huyo na kumtekeleza barabarani. Hadi hivi sasa bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari kwani haijulikana alileweshwa kwa dawa gani.

error: Content is protected !!