Pambano kali kati ya Putin na Elon Musk

HomeKimataifa

Pambano kali kati ya Putin na Elon Musk

Tajiri mkubwa duniani Elon Musk, ameibua mjadala katika mitandao ya jamii baada ya kuandika kupitia ukurasa wake wa twitter kuwa anaomba pambano la ngumi kati yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Katika ujumbe wake huo alisema kuwa mtu atakayeshinda katika pambano hilo basi atakua na mamlaka juu ya taifa la Ukraine.

Elon hakuishia hapo alimuuliza kama Putin yuko tayari kwa pambano hilo, Kwa upande wa Putin hakujibu chochote kuhusu ombi hilo la Elon.

Kwa upande wa ngumi Putin ana mkanda mweusi wa Judo na alikuwa kiongozi wa Judo nchini Urusi.

Baadae shirikisho la Kimataifa la Judo na Shirikisho la Judo la Ulaya lilithibitisha kumsimamisha Putin katika majukumu yake kama rais wa heshima na balozi wa judo baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kwa upande wa Elon aliwahi kujifunza mapigano nchini Brazil pia ana uzoefu kwenye Karate, judo na Taekwondo.

Lakini kwenye  maisha ya kawaida Elon ni tajiri mkubwa duniani mwenye uraia wa Afrika Kusini, Canada na Marekani pia ni mjasiriamali na mmiliki wa kampuni ya magari ya Tesla, Kampuni ya roketi za anga Space X na muanzilishi wa huduma ya Paypal.

Watu wengi walimpa nafasi kubwa Elon Musk ya kushinda kwa kigezo cha umri, urefu na uzito, Kwa upande wa umri Elon ni mdogo zaidi kwa Putin kwa tofauti ya miaka 19.

Kwenye urefu Elon ana urefu wa futi 6 na inch 2 huku Putin akiwa na urefu wa futi 5 na inchi 5 na kwenye kilo Elon ana kilo 80 na putin ana kilo 70.

error: Content is protected !!