Huyu ndiye mwanzilishi wa chama kipya cha Umoja

HomeKitaifa

Huyu ndiye mwanzilishi wa chama kipya cha Umoja

Imebaki miaka minne kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 nchini Tanzania. Chama kipya cha siasa kilijulikano kama Umoja Party (UP) kimeibuka kuomba usajili wa muda. Chama hicho tayari kimewasilisha maombi ya usajili wa muda ili kuanza kutafuta wadhamini kwa lengo la kupata usajili wa kudumu. Mwenyekiti wa chama hicho kitakachokuwa na makao makuu yake Dar es Salaam, Seif Maalim Seif amesema kuwa dira cha chama chake ni kuondoa umasikini Tanzania.

SEIF MAALIM SEIF NI NANI?

Mwaka 2020 Seif Maalim Seif aligombea nafasi ya urais kupita Chama cha Wakulima (Alliance for Africa Farmers Party). ambapo kupitia chama hicho mwaka 2020 Seif Maalim Seif alijipambanua kwa itikadi ya Uchumi wa Kilimo (Agricultural-based economy). Taarifa zinaonesha kuwa Seif Maalim Seif ana umri wa miaka 47. Seif anasema kuwa ni umoja pekee ndio unaweza kutatua matatizo ya nchi hii ndio maana Chama hicho kinaitwa Umoja.

Seif ni muumuni wa siasa za utulivu na kuleta mabadiliko kwa njia za majadiliano. Kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 aliwahi kunukuliwa akipinga vikali siasa za kusambaza maneno ya uchochezi ambayo yangehatarisha amani nchini. Seif alisema kuwa vyama vyote vina lengo moja la kuongoza dola, hivyo basi lazima vifanye siasa za kiungwana, pasi kuchochea vurugu kwani Tanzania ni moja na hakuna nyingine.

> Nafasi za kazi Hindu Mandal Hospital

ITIKADI YA CHAMA CHA UMOJA

Chama cha Umoja kinajipambanua kiitikadi kuwa kinaazimia kutumia utajiri wa rasilimali uliopo Tanzania kunufaisha wananchi kwanza na kutatua tatizo kubwa la ajiri linalowakabili watanzania. Kupitia bendera yake yenye rangi nyeupe, nyeusi, dhahabu pamoja na kijani, Seif Maalim Seif amesema kuwa nyeupe ina maana ya amani, uwazi na upendo, na kijani ni rasimali za nchi yetu, nyeusi ni uafrika wetu pamoja na dhahabu ni tafsiri kuwa nchi ya Tanzania imebarikiwa rasilimali ya madini.

Naibu Msajili wa vyama vya siasa nchini, Sisy Nyahoza amethibitisha kuwapo kwa maombi ya usajili wa Chama hicho mezani kwake, na kwamba sheria ya vyama vya siasa inawataka kutangaza kwenye gazeti la Serikali na kutoa muda kwa wananchi pamoja na vyama vya siasa kupinga jina la chama kwa ofisi ya msajili. Baada ya mchakato huo kumalizika, hatua nyingine zitafuata kama sheria inavyoelekeza

Seif Maalim Seif si mgeni kwenye siasa za Tanzania, kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 Seif aligombea nafasi ya urais kupitia Chama cha Wakulima (AAFP).

error: Content is protected !!