EAC yatahadharisha magonjwa ya mlipuko

HomeKimataifa

EAC yatahadharisha magonjwa ya mlipuko

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imezitaka nchi za wanachama wake kuongeza kasi ya kuzuia na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika kipindi cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hii ni baada ya mlipuko wa homa ya manjano nchini Kenya iliyosababisha vifo vya takribbani watu watatu.

“Mvua kubwa na joto kali vimesababisha idadi kubwa ya mbu wanaoambukiza magonjwa yanayoenezwa na wadudu,” alisema Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia sekta za uzalishaji na jamii, Christophe Bazivamo.

Bazivamo alisema pia kuwa mlipuko wa homa ya bonde la ufa unaweza kufuatiwa na madhara kwa binadamu endapo hatua za kutosha hazitachukuliwa mapema.

Aidha, alizitaka nchi wanachama wa EAC kuripoti milipuko hiyo kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Kimataifa la Afya ya Wanyama (OIE) kama inavyotakiwa, sambamba na kuongeza ufuatiliaji, udhibiti na chanjo dhidi ya homa ya manjano miongoni mwa raia. 

error: Content is protected !!