Tanzania yapeleka helikopta mbili za msaada Malawi

HomeKitaifa

Tanzania yapeleka helikopta mbili za msaada Malawi

Serikali ya Tanzania imetuma helikopta mbili nchini Malawi zenye msaada wa vifaa, chakula pamoja na fedha Dola milioni moja (Sh. bil. 2.3) taslimu kwa ajili ya kusaidia walioathiriwa na kimbunga Freddy, nchini humo.

Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gaudentius Ilonda, alisema : “Helikopta mbili zimeruka kutoka Dar es Salaam kwenda Malawi kusaidia shughuli za uokoaji katika maafa yanayoendelea.

” Pia serikali imetoa vifaa kama blanketi na mahema na shehena za chakula zitapelekewa kila siku mpaka kufikia tani 1000,” alisema.

Balozi wa Tanznaia nchini Malawi, Humphrey Polepole, alithibitisha kupokewa kwa msaada huo na kwamba Serikali ya Tanzania, itaendelea kusaidia nchi hiyo katika kipindi hiki kigumu.

 

error: Content is protected !!