Ajinyonga kisa kunyimwa mshahara

HomeKitaifa

Ajinyonga kisa kunyimwa mshahara

Ofisa Muuguzi (II) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, Dar es Salaam, Sarwat Soluwo amedaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kilichodaiwa mateso aliyopitia baada ya kusimamishiwa mshahara na uongozi wa hospitali hiyo.

Taarifa za ndani ya hospitali hiyo zinaeleza Sarwat alisitishiwa mshahara kwa miezi michache iliyopita kutokana na tabia ya ulevi huku akihitajika kuendelea na kazi bila ya mshahara.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alithibitisha kutokea kwa tukio la kujinyonga kwa kijana huyo na kusema uchunguzi unaendelea.

Kwa mujibu wa taarifa, baada ya kufanya kazi kwa muda bila mshahara , adhabu hiyo ilimuathiri na kugeuka ombaomba hospitalini hapo, ili apate fedha za kula pamoja na za kumuwezesha kufika kazini.

“Hali ilizidi kuwa ngumu kwake, akaanza kuuza vyombo vya ndani, ili apate kula na nauli, kuna kochi alinunua fedha nyingi aliuza Sh60,000 kwa sababu ya ugumu wa maisha na alizidisha unywaji wa pombe zaidi.

“Baada ya kulewa kuna watu walimdhuru akaletwa hospitali alivyorudi nyumbani kwake hali ile ikamkwaza akachukua uamuzi wa kujinyonga,” alidai mfanyakazi mwenzake.

 

 

error: Content is protected !!