Karia atia neno Siku ya Wananchi

HomeMichezo

Karia atia neno Siku ya Wananchi

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameipongeza Yanga kumualika Kocha mkubwa Afrika Pitso Mosimane na kwamba amesikia Simba nao wamemualika Rais wa CAF kwenye siku yao ya Simba Day.

“Nawapongeza Yanga kumualika kocha mkubwa Afrika, Pitso Mosimane pia nimesikia Simba nao wamemualika Rais wa CAF lakini sina uhakika kama tayari amethibitisha kuwepo kwake.

“Nilitamani kuwepo leo kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi lakini nimeshindwa kutokana na majukumu niliyonayo huku jijini Arusha ya Mkutano Mkuu wa CAF, niwatakie kila la kheri kwenye siku yao hii, wakaonyeshe dunia ukubwa wa soka la Tanzania.

“Niwaombe Wanayanga kuondoa tofauti zao na kuachana na taarifa za mitandao ya kijamii mimi nitabaki kusimamia mpira wa Tanzania bila kuwa na upendeleo.” amesema Karia akizungumza TBC leo.

 

 

error: Content is protected !!