Matunda ziara ya Rais Samia nchini China na Misri

HomeKitaifa

Matunda ziara ya Rais Samia nchini China na Misri

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, amezungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais Samia nchini China na Misri.

Zuhura amesema Tanzania na China zimeahidiana kuendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali yenye kuleta tija na manufaa pande zote.

Ushirikiano huo ni kwenye sekta ya uchumi ambapo China ameahidi kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka Tanzania, kuongeza uwekezaji nchini ambapo fursa nyingi za ajira zinatarajiwa kupatikana, Ujenzi wa viwanda ili kuongeza uwezo wa uzalishaji na usindikaji nchini.

Pia wamekubaliana kutotoza ushuru kwa 98% kwa bidhaa kutoka Tanzania kwenda China, kukuza uchumi wa kidijitali, uchumi wa buluu na kushirikiana katika mradi wa kufufua reli ya TAZARA.

China pia imeahidi kushirikiana na Tanzania kiuchumi ambapo sasa Tanzania itaanza kuuza parachichi nchini China pamoja na mabondo.

Aidha, katika ziara hiyo China na Tanzania zilitia saini za makubaliano katika mambo mbalimbali kama kujenga makumbusho ya kisasa, ushirikiano wa kujenga uchumi wa kidigitali, kuongeza ununuzi wa maparachichi na mabondo ya samaki na mkopo wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege Zanzibar pamoja na hati za vifaa vya upekuzi.

Mwaka 2024 Tanzania na China zitatimiza miaka 60 ya ushirikiano na hivyo kukubaliana kutumia diplomasia kukuza  zaidi sekta ya utalii.

MISRI

Mkurugenzi huyo wa Mawasiliano ya Rais Ikulu amesema ,Rais akiwa nchini Misri kushiriki mkutano wa COP27, alipata fursa ya kukutana na baadhi ya marais kujadili nishati ya umeme ambapo Benki ya Dunia imekubali kutoa dola bilioni 18 katika uwekezaji wa nishati jadidifu.

 

 

error: Content is protected !!