Wafukua kaburi na kuiba sehemu za siri za marehemu

HomeKitaifa

Wafukua kaburi na kuiba sehemu za siri za marehemu

Watu wasiojulikana wamefukua kaburi alipokuwa amezikwa marehemu Ruben Kasala (74) na kuondoa sehemu za siri.

Mtoto wa marehemu, Frank Kasala amesema tukio hilo limetokea Machi 19, 2023 katika Kijiji cha Kasokola Kata ya Kasokola Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Frank amesema baba yao alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari na pia alikuwa na shida kwenye mapafu lakini ilipofika siku ya tarehe 18 asubuhi, walipokea taarifa ya msiba na siku hiyohiyo wakafanya shughuli za maziko.

“Kama ilivyo taratibu mnapozika asubuhi lazima wanafamilia mrudi makaburini baada ya kurudi tukakuta kaburi limechimbwa na mwili wa baba yetu umefukuliwa, sanduku limevunjwa kabisa, wakavuta sanduku wakatoa kisha wakarudisha wakafukia kidogo na udongo, hatujajua nini kilichofanyika tunasubiri uchunguzi wa serikali ili kujua kilichofanyika,” amesema Frank Kasala.

 

source: HABARI LEO

error: Content is protected !!