Hii hapa Ramani mpya ya EAC

HomeBiashara

Hii hapa Ramani mpya ya EAC

Rais Uhuru Kenyatta, Paul Kagame na Yoweri Museveni wa Kenya, Rwanda na Uganda mtawalia, leo Aprili 6, wamezindua ramani mpya ya Jumuiya Afrika Mashariki inayoijumuisha mwanachama wake mpya.

Katika Ikulu ya Kenya jijini Nairobi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Tshisekedi amesaini mkataba wa kujiunga rasmi na jumuiya hiyo.

Kuiongeza DRC kuwa mwanachama wa EAC kutaimarisha uchumi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo, amesema Rais Kenyatta ambaye pia ndiyo Mwenyekiti wa EAC.

“Kwa ndugu yangu na rafiki yangu Rais Tshisekedi na kwa watu wa DRC, tunawakaribisha katika Umoja wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hizi mbili ndizo nguzo sahihi za jumuiya yetu na msingi ambao maslahi ya kijamii, kisiasa, biashara, uwekezaji na kiuchumi yanasimama,” ameongeza Rais Kenyatta.

 

error: Content is protected !!