Mtoto wa kigogo afariki akimuokoa mpenzi wake

HomeKimataifa

Mtoto wa kigogo afariki akimuokoa mpenzi wake

Juan Carlos Escotet Alviarez mtoto wa bilionea wa Uhispania Juan Carlos Escotet Rodriguez amefariki dunia katika jitihada za kuokoa maisha ya mkewe mtarajiwa aliyeangukia baharini.

Wawili hao walikuwa wakishiriki mashindano ya uvuvi huko Florida wakati Andrea Montero (30) alipoanguka kwenye maji urefu wa futi 60 na kupelekea Alviarez kuruka kwenye maji kumuokoa na kuangukia upanga uliopelekea majeraha yaliyopelekea umauti wake.

Alviarez (31) na Montero walikuwa wakitarajia kufunga ndoa mwezi Novemba mwaka huu.

Baba wa Alviarez ambaye pia ni mmiliki wa benki ya Banesco anatajwa kuwa na utajiri wa dolo za kimarekani bilioni 3.5 sawa na shilingi bilioni 810. 6.

Montero alifanikiwa kutoka salama ndani ya maji bila majeraha yoyote.

error: Content is protected !!