Mange Kimambi apata pigo

HomeBurudani

Mange Kimambi apata pigo

Zaidi ya wafanyakazi 10 wa Mange Kimambi app wamekamatwa na polisi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mtandao kutokana na video iliyowekwa kwenye mtandao huo majuma yaliyopita ikimuonyesha aliyewahi kuwa Mbunge wa Mikumi, Profesa Jay akiwa hospitali.

Video hiyo iliibua hisia kwa watu wengine na kulaani kitendo hicho cha kusamabaza picha zikimuonyesha Profesa Jay ambaye amelazwa Muhimbili akiwa katika hali ambayo sio nzuri.

Taarifa za kukamatwa kwa wafanyakazi hao imetolewa na Mange baada ya kuchapishwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram nakusema kuwa yeye hawezi kumtaja mtu aliyemtumia video hiyo hivyo kuwataka polisi kuwaachia watu wake.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Mange Kimambi (@mangekimambi_)

error: Content is protected !!