Hali ya Watanzania waliopo Ukraine

HomeKimataifa

Hali ya Watanzania waliopo Ukraine

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa Watanzania wote waliokuwa wamekwama nchini Ukraine kutokana na vita inayoendelea wameondoka salama.

“Utaratibu wa kuwaondoa umekamilika na Watanzania 300 waliokuwepo Ukraine wote wameondoka kuelekea nchi jirani na baadhi yao wamerejea nchini,” alisema Balozi Mulamula.

Mchakato huo wakuwaondoa umefanikiwa kupitia balozi zake za Ujerumani na Sweden zilizofanya uratibu wa kuwatoa raia wa Tanzania nchini humo hususani wengi wao waliokuwa wamekwama mpakani mwa Ukraine na Urusi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita, Balozi Mulamula ametoa wito kwa Watanzania wote waliopo nje ya nchi kuhakikisha wanajiadnikisha ubalozini ili kurahisisha uratibu endapo itahitajika

error: Content is protected !!