Mume aua mke na mtoto kisa mchele

HomeKitaifa

Mume aua mke na mtoto kisa mchele

Jeshi la polisi linawashikilia wanaume wawili wakazi wa Nkungwi, Katavi kwa mauaji ya watu wawili.

Dutu Maige akishirikiana na Yusuph Sita wanadaiwa kumuua Mariamu Paschal (36) na mwanae Editha Dutu (4) ambao ni mke na mtoto wa Maige na kuwafukia kwenye shimo.

Baba mzazi wa Mariamu aliripoti polisi kuwa bintiye na mjukuu wake wametoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu Julai 2021 na msako wa kuwapata ukaanza mara moja.

Watuhumiwa hao walikamatwa na kukiri kutekeleza mauaji hayo na kuwapeleka polisi walipohifadhi miili hiyo katika pori la Kalilankulunkulu, eneo la shamba la Magereza ya Tanganyika.

Chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia kati ya Maige na mkewe juu ya magunia 60 ya mpunga.

Jeshi la polisi bado linaendelea na upelelezi wa kesi hii. na baadaye kuwafikisha watuhumiwa hao kizimbani

error: Content is protected !!