Agizo la mahakama kwa aliyesambaza picha za ngono WhatsApp

HomeKitaifa

Agizo la mahakama kwa aliyesambaza picha za ngono WhatsApp

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata Faraji Omary mwenye umri wa miaka 26 kwa kutotokea mahakamani bila kutoa taarifa.

Faraji anashutumiwa kwa kosa la kusambaza picha za ngono kwenye mtandao wa WhatsApp ambalo anadaiwa kulitenda kati ya Desemba 4 na 14 mwaka 2020.

Licha ya kushtumiwa kutenda kosa hilo, Faraji na mwenzie Aisha Kiula mwenye umri wa miaka 22 maarufu kama Sex Aysher wanakabiliwa na mashtaka saba ikiwemo kuandaa sherehe ya ufuska, kusambaza picha za ngono kwenye mtandao wa kijamii pamoja na kusambaza tiketi zenye ujumbe unaoharibu maadili ya umma.

Sherehe ambayo Omary na Aisha walipanga kuifanya ilikua ifanyike maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambapo mhudhuriaji alitakiwa kununua tiketi ambayo ingemuwezesha kuingia katika nyumba maalum iliyokuwa na wanawake wa kustarehe nao kwa idadi ambayo inalingana na  thamani ya tiketi ulionunua.

Tiketi zilizokuwa zinauzwa ni kuanzia Tsh 150,000 ambayo ingemfanya mwanaume kupata mwanamke mmoja na chupa moja ya pombe kali au mvinyo na Tsh 300,000 mwanaume angepata wanawake wawili wa kufanya nao ngono pamoja na chupa mbili za pombe kali au mvinyo.

error: Content is protected !!