Gomes atupiwa virago Simba

HomeMichezo

Gomes atupiwa virago Simba

Klabu ya Simba imeridhia ombi la aliyekuwa Kocha Mkuu, Didier Gomes da Rosa la kuachana na timu hiyo kuanzia leo tarehe 26.10.2021

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza kuwa baada ya tathmini na majadiano ya kina, pande zote zimeafikiana kwa mujibu wa mkataba na manufaa ya wote na kutokana na hatua hiyo, aliyekuwa Kocha msaidizi, Thierry Hitimana, ndiye atakuwa Kocha Mkuu wa Simba katika kipindi hiki cha mpito akisaidiwa na Selemani Matola.

Aidha, Klabu pia imefanya mabadiliko madogo katika benchi la ufundi kwa kusitisha mikataba ya aliyekuwa Kocha wa Makipa, Milton Nienov na Kocha wa Viungo, Adel Zrane.

Klabu ya Simba imeeleza kuwa inamshukuru Kocha Gomes na wenzake kwa mafanikio waliyopata katika kipindi walichoitumikia Simba na kuwatakia heri katika majukumu yao mengine huko waendako.

error: Content is protected !!