Aua kwa panga kisa wivu wa mapenzi

HomeKitaifa

Aua kwa panga kisa wivu wa mapenzi

Mkazi wa Kijiji cha Mgombani, SWilaya ya Monduli mkoani Arusha, Juma Ndaji (27), anashikiliwa na polisi wilayani humo kwa kosa la kumkata panga mfanyabiashara, Paulo Akwesso (58) na kumsababishia kifo chake, akimtuhumu kuwa na uhusiano na mpenzi wake.

Mtuhumiwa huyo pia inadaiwa alimjeruhi kwa panga Rebeka John (22), anayesadikiwa kuwa ni mpenzi wake, ambaye amelazwa Kituo cha Afya Mto wa Mbu kwa matibabu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa nne usiku Kitongoji cha Kirurumo, Kata ya Majengo, kwenye chumba cha mwanamke huyo.

Akifafanua chanzo cha tukio hilo ni mtuhumiwa, kumtuhumu marehemu kuwa na uhusiano na mpenzi wake, ambaye pia alijeruhiwa kwa panga baada ya kuwakuta chumbani.

error: Content is protected !!