Mama azaa watoto wanaobadilika jinsia

HomeKitaifa

Mama azaa watoto wanaobadilika jinsia

Mama mmoja kutoka Bukoba mwenye umri wa miaka 43, jina lake limehifadhiwa amekumbwa na sintofahamu baada ya  watoto wake watatu aliowazaa kuwa na jinsia tata.

Mama huyo anasema ameishi na changamoto hiyo kwa watoto wake kwa muda wa miaka 19 watoto hao huzaliwa na jinsia ya kike lakini baadae huwa na jinsia ya kiume.

Mtoto wa kwanza wa mama huyo alizaliwa akiwa wakike na kulelewa kama mtoto wa kike, Mabadiliko yalianza kujitokeza akiwa na umri wa miaka 8 na baadae akaanza kuwa na matendo kama ya kiume na hatimaye akaja kuota jinsia ya kiume na kufanya kuwa na jinsia mbili ya kike na kiume.

Wakati mabadiliko hayo yanaendelea tayari alikua amejifungua mtoto wa pili.Mtoto wake wa pili na watatu baadaye pia walianza kubadilika jinsia na kuota jinsia ya kiume pamoja na mabadiliko ya sauti kutoka ya kike hadi ya kiume, watoto hao wanatoa haja ndogo kupitia maumbile yao ya kike ambayo ndo walizaliwa nayo.

Mama huyo ana watoto wengine wanne ambao wana hali ya kawaida watatu wa kiume na mmoja wa kike.Moja kati ya watoto hao amebahatika kupata matibabu baada ya kufanyiwa vipimo na kugundulika jeni zake nyingi ni za kiume, Hivyo ilibidi abadilishwe jina na kuitwa jina la kiume licha ya kuishi miaka 14 kama mwanamke.

Kijana huyo ameomba ndugu zake ambao bado hawajapatiwa matibabu waweze kupatiwa msaada.Daktari bingwa wa uzazi, Dk Joshua Gerison anasema hali hiyo insababaishwa na hitilafi za kimaumbile yao au jeni, Mtoto mwenye shida ya jinsia huzaliwa akiwa na vinasaba vinavyozidi 46 kipimo ambacho kinatakiwa ili jinsia ya mtu itambulike vyema.

error: Content is protected !!