Sokwe dume mzee zaidi duniani, afariki akiwa na umri wa miaka 61 katika Zoo Atlanta

HomeKimataifa

Sokwe dume mzee zaidi duniani, afariki akiwa na umri wa miaka 61 katika Zoo Atlanta

Sokwe dume mzee zaidi duniani anayefahamika kwa jina la Ozzie, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61 katika hifadhi ya wanyama nchini Atlanta huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijajulikana.

Wasimamizi wa hifadhi hiyo wakisema kwamba masaa 24 kabla Ozzie alitoka kutibiwa uvimbe wa uso, udhaifu wa kula na kunywa.

Maafisa wa hifadhi hiyo walisema, Ozzie alikuwa ni mmoja wa Sokwe 13 katika hifadhi ya Atlanta ambaye aliambukizwa Uviko-19 mwaka jana huku ikiaminika kwamba sokwe huyo aliipata kutoka kwa mfanyakazi wa hifadhi hiyo.

Ozzie alikuwa na uzito wa pauni 350 na alifika kwenye bustani ya wanyama mwaka 1988, alizaa sokwe 12 katika bustani hiyo ambapo Mkurugenzi wa hifadhi hiyo Raymond King alimtaja kama “baba wa kutisha” kwa kuwa hakupenda muziki wa sauti kubwa .

“Hii ni hasara kubwa kwa hifadhi ya  Atlanta ingawa tulijua wakati huu ungefika siku moja, lakini tusingeweza kufanya chochote kuepeuka kuzuia huzuni kama hiyo tuliyoipata,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa hifadhi, Raymond King.

error: Content is protected !!