Aliyemwagiwa tindikali aomba msaada

HomeKitaifa

Aliyemwagiwa tindikali aomba msaada

Tark ni kijana mdogo wa kitanzania, mzalendo na aliekuwa na ndoto zake kubwa lakini leo ndoto hizo zimefifia, matumaini yamepotea, baada ya kuvamiwa na vijana wawili waliokuwa kwenye bodaboda na kumwagiwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni tindikali, tarehe 5 mwezi March 2022 akiwa Moshi mkoani Kilimanjaro.

Hali hiyo imepelekea kuharibu uwezo wake wa kuona kawaida na kumsababishia majeraha makubwa usoni pamoja na mikononi.

Kwa sasa kijana wetu Tark anaendelea na matibabu katika hospitali ya KCMC Moshi, wakati akisubiri kupelekwa India kwa matibabu zaidi.

Kutokana na gharama za matibabu kuwa kubwa na familia yake kushindwa kumudu gharama hizo kwa wakati, tunaomba watanzania wenye nia njema na wale watakaoguswa kuungana na familia yake kufanikisha michango kwa hiyo, kwa ajili ya matibabu ili kijana wetu aweze kurejesha tabasamu usoni na kuona tena na hatimaye kutimiza ndoto zake.

Gharama za matibabu nchini India ni dola Elfu 15 ( $ 15,000/= ) sawa na shilingi za kitanzania milioni 35.

Tark anatarajiwa kwenda India kwa matibabu zaidi ikiwemo upasuaji ambao tunaamini kwa mapenzi ya Mungu matibabu hayo yatamsaidia kurudi katika hali ya kawaida na kuona na kuponya majeraha aliyoyapata.

Kwa yeyote atakaewiwa na kuguswa kumchangia kijana Tark ,mchango utumwe kwa namba zifuatazao.

Mpesa *0764 51 07 74* Jina Tark Kipemba.
Au account namba : *3012111594790*
Jina la Mwenye account : Tariq Kipemba
Jina la bank : Equity Bank.

Tunatanguliza shukurani za dhati kwenu nyote, na Mungu azidi kuwabariki

Familia ya Tark Kipemba.

 

SOURCE: CLOUDS TV

error: Content is protected !!