8 wafariki, ajali ya basi la shule

HomeKitaifa

8 wafariki, ajali ya basi la shule

Watu nane wamefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea mkoani Njombe kati ya basi la shule aina ya coaster na lori.

Coaster hiyo yenye namba za usajili T287 CCY, mali ya Kanisa Katoliki lilikuwa limebeba baadhi ya waumini ikiwemo wanachama wa Umoja wa Vijana Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe (UVIKANJO)  iligonganana Lori lililokuwa limebeba makaa ya mawe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika Barabara kuu ya kuelekea Ruvuma katika eneo la Igima wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe.

Aidha, amewataja waliofariki kuwa ni  Flora Mkinga, Veronica Mwinuka, Teresia Mbuligwe, Alfred Mfuse, Benson Kigahe, Mariamu Mkulu, Eliezer Mwakipesile, na Frida Msigwa.

Majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea jana jioni wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospital ya Rufaa ya Njombe pamoja na hospitali ya Mji wa Njombe Kibena.

error: Content is protected !!