Makamba atoa sababu za kutokuwepo bungeni

HomeKitaifa

Makamba atoa sababu za kutokuwepo bungeni

Waziri wa Nishati January Makamba amelazimika kuomba radhi ndani ya Bunge kufuatia kusababisha bunge kusimama kwa dakika 30 asubuhi baada ya yeye na Naibu Waziri wake Stephen Byabato kutokuwepo bungeni wakati mjadala wa wizara hiyo ukiendelea.

Waziri Makamba ameeleza kuwa kutokana na uzito wa hoja zilizotolewa na wabunge hao jana iliwalazimi yeye na Naibu wake kuamkia katika kikao cha kutafuta majibu ya hoja zao huku wakiamini kuwa muda wa maswali na majibu utamalizika saa nne na robo asubuhi na badala yake ukamalizika kabla ya saa nne.

“Kosa tulilofanya ni utabiri na tulichojifunza ni utabiri, utabiri kwamba maswali huwa yanaisha saa nne na dakika 10 au 15 kutokana na uzoefu wetu, kumbe leo yameisha kabla ya saa nne, kwahiyo tunaingia tunapishana na msafara unatoka, tukatamani kuingia chini ya viti, lakini tunashukuru kwa uelewa wa bunge na tumejifunza kuanzia leo hatutatabiri tena” ameeleza Makamba.

Bunge lilihairishwa kwa muda wa nusu saa kufuatia tangazo lililotolewa na Mwenyekiti wa Bunge, David Kihenzile bungeni jijini Dodoma leo asubuhi.

 

 

error: Content is protected !!