Kim: Nipo tayari kula kinyesi nibaki kuwa kijana

HomeBurudani

Kim: Nipo tayari kula kinyesi nibaki kuwa kijana

Mwanamitindo maarufu duniani Kim Kardashian ameshangaza wengi baada ya kusema kwamba yupo tayari kula kinyesi kama kinaweza kumsaidia kuonekana kijana kila siku.

Mama huyu wa watoto wanne, North West, Chicago West, Psalm West na Saint West amesema hayo alipokuwa kwenye mahojiano na kituo cha The NewYork Times kwamba yupo tayari kufanya na kula chochote ili aendelee kuonekana kijana.

“Ikiwa utaniambia kwamba inapaswa nile kinyesi ili nibaki kuwa kijana basi ningefanya hivyo,” alisema Kim.

Aidha, Kim mwenye miaka 41 amesema wapo watu wanaojifanya kutojali mabadiliko katika miili yao ikiwemo kuzeeka, kwake yeye ni tofauti na ndio maana yupo tayari kwa lolote.

error: Content is protected !!