Mbunge adhamini walimu kutalii mbugani

HomeKitaifa

Mbunge adhamini walimu kutalii mbugani

Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amedhamini ziara ya siku mbili ya walimu wa sekondari na shule za msingi kwenda kutalii kwenye mbuga za wanyama hapa nchini kama sehemu ya kuhamasisha kampeni ya utalii wa ndani na kuunga mkono juhudi za Rais, Samia Suluhu Hassan katika suala la utalii.

Walimu hao watatembelea mbuga ya Wanyama ya Ruaha mkoani Iringa kwa lengo la kujifunza zaidi juu ya vivutio vya Uutalii nchini sambamba. Mavunde ameeleza kuwa pia ziara hiyo ni sehemu ya motisha kwa walimu kwa kazi kubwa wanayofanya.

error: Content is protected !!