Ufafanuzi wa laki 8 ya kuunganisha umeme

HomeKitaifa

Ufafanuzi wa laki 8 ya kuunganisha umeme

Wizara ya Nishati imesema gharama halisi ya kuunganisha huduma ya umeme katika nyumba kwa wakazi wa mijini na vijijini ni Sh800,000.

Hata hivyo, kiasi hicho hakitolewi na wananchi kama inavyodaiwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii.

Serikali imekuwa ikitoa ruzuku ili kupunguza gharama hiyo ili kuwawezesha Watanzania kuipata kwa urahisi kuwawezesha kutekeleza shughuli za maendeleo.

Waziri wa Nishati, January Makamba aliyekuwa akizungumza Septemba 5, 2022 katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, alisema fedha hizo zingekuwa zinatolewa na wananchi zingesaidia  kuboreshea huduma zingine ikiwemo kupanua mtandao wa umeme.

“Mwananchi akitakiwa kulipa Sh 27,000 ajue Serikali inachangia Sh773,000 kutoka kwenye mfuko wake na tukisema mteja alipe Sh321,000 kwa kiwango hicho ajue Serikali inachangia Sh 489,000, ni muhimu lijulikane hili.

Amesema gharama halisi za umeme na kuunganishiwa ni bei ambazo zinawekwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kwa hiyo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) haliwezi kutoza kiwango zaidi ya kilichopangwa na mamlaka husika.

Amesema Tanesco inaingia gharama za kununua waya, mita na nguzo ambazo hutumika kumuunganishia mteja umeme.

error: Content is protected !!