Auawa baada ya kubaka mbuzi

HomeKitaifa

Auawa baada ya kubaka mbuzi

Kijana mmoja kutoka Mtunzini huko KwaZulu-Natal, Afrika Kusini ameuawa kutokana na kichapo cha wananchi wenye hasira kali baada ya kumfuma akibaka mbuzi.

Tukio hilo lilitokea Septemba 5, 2022. Kwa mujibu wa 1KZNTV News, mwanaume huyo alitaka kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 61 alipojaribu kuingia ndani ya nyumba yake, hata hivyo mwanamke aliweza kujitetea na kumtishia kumkata kichwa iwapo ange jaribu.

Kijana huyo aliamua kuhamishia hasira zake kwa mbuzi, inadaiwa mwanamke aliitisha yowe na raia walimkuta kijana akiwa bado juu ya mbuzi ambapo walijichukulia sheria mkononi kwa kumpiga hadi kifo.

error: Content is protected !!