Mtanzania Abby Chams kwenye show kubwa ya ‘Kelly Clarkson

HomeBurudani

Mtanzania Abby Chams kwenye show kubwa ya ‘Kelly Clarkson

Kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani binti wa Kitanzania Abby Chams ambaye ni mwanamuziki amepata nafasi ya kuwakilisha Wasichana wa Tanzania kwenye kipindi kikubwa nchini Marekani kinachojulikana kwa jina la ‘Kelly Clarkson Show.’

Abby ameweza kuonekana katika kipindi hicho kutokana na jitihada zake kwenye kipindi chake cha ‘Teen Talk with Abby Chams’ alichokianzisha mwaka 2019 kilichobeba dhumuni kubwa la kuwaelimisha vijana wadogo kuhusu matatizo wanayokutana nayo na jinsi wanayoweza kukabiliana nayo.

Mwaka 2020, Abby alichaguliwa na Mfuko wa Kimataifa wa Watoto (UNICEF), kama mtetezi wa vijana akiwakilisha Tanzania.

Kupitia ukurasa wake Instagram Abby amewasihi wasichana wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii akiwasihi kujiamini na kuamini nguvu iliyo ndani yao kwani kwa jitihada siku moja wanayoyafanya yataonekana. #clickhabari

error: Content is protected !!