IGP Sirro ahamisha Makamanda wa mikoa watatu

HomeKitaifa

IGP Sirro ahamisha Makamanda wa mikoa watatu

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi imeeleza kuwa Mkuu wa Jeshi hilo nchini, IGP Simon Sirro  tarehe 4/10/2021 alifanya mabadiliko ya Makamanda watatu kwa kuwabadilisha mikoa.

Waliohamishwa ni Kamishna Msaidizi wa Polisi Blasius Chatanda ambaye amehamishwa kutoka mkoa wa Tanga kwenda mkoa wa Simiyu. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi Richard Abwao amehamishiwa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi Safia

Shomari ambaye amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uhamisho uliofanyika ni wa kawaida wenye lengo la kuboresha ufanisi katika kutekeleza jukumu la kulinda maisha ya watu na mali zao.

error: Content is protected !!