Zijue aina za habari ambazo huruhusiwi kuweka  Facebook sasa

HomeKimataifa

Zijue aina za habari ambazo huruhusiwi kuweka Facebook sasa

Mtandao wa Facebook unawatumiaji bilioni 2.85 kila mwezi. Watumiaji wa mtandao huo huutumia kwa matumizi mbalimbali kama kutangaza biashara, kuwasiliana na hata kuuza na kununua bidhaa.

Kumekuwa na ongezeko kubwa sana katika mtandao huo kutumika kama silaha ya kuchafua watu wengine, kutuma na kupokea picha chafu na pamoja na mtandao huo kutumika kama jukwaa la matusi dhidi ya watu maarufu kama wasanii, wanamichezo pamoja na viongozi wa nchi mbalimbali.

Kampuni ya Facebook imesema itakuwa itachukua hatua madhubuti kuzuia maudhui ya watu yanayolipiwa kwa malengo ya kuchafua watu wengine.

Kiongozi wa usalama viongozi, Antigone Davis amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa maboresho ya sera ya Facebook katika kudhibiti matusi, udhalilishaji na dhihaka kutoka kwa mtu mmoja kuenda kwa mtu mwingine katika mtandao huo.

Ifuatayo ni aina ya maudhui ambayo yatapata adhabu ya kufungiwa:

  1. Maudhui ya utupu wa kupindukia
  2. Wasifu, kurasa, makundi na matukio yanayowekwa Facebook ambayo yanadhamiria kuchafua watu maarufu.
  3. Picha zilizohaririwa na programu tumishi kama ‘Adobe Photoshop’ zenye lengo la kuchafua taswira ya mtu.
  4. Mashambulizi yanayofanywa kwa mtu, kwa kudhihaki maumbile yake, kwa kumtaga na kumtag moja kwa moja mtu husika.
error: Content is protected !!