Bandari ya Mtwara yaanza kusafirisha makasha

HomeKitaifa

Bandari ya Mtwara yaanza kusafirisha makasha

Bandari ya Mtwara Mkoani Mtwara imezindua huduma ya meli ya kusafirisha makasha. Huduma hizo zimezinduliwa leo Aprili 20, 2023 na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete kupitia Meli ya Kampuni ya CMA-CGM kutoka Dubai.

Meli hiyo yenye urefu wa mita 176.88 na uwezo wa tani 18,485 itahudumia shehena itakayosafirishwa kwenda Moroni na Mutsamudu Visiwa vya Comoro. Meli hiyo imetia nanga katika gati jipya ikiwa imebeba makasha 246 na itatarajiwa kukaa gatini kwa muda usiozidi saa 24 kwa ajili ya kushusha makasha hayo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma hizo, Mwakibete amesema ujio wa meli hiyo ni fursa kwa Bandari hiyo kufungua milango ya meli nyingine zaidi kuja.

error: Content is protected !!