Mbivu na mbichi kesi ya kina Mbowe kujulikana leo

HomeKitaifa

Mbivu na mbichi kesi ya kina Mbowe kujulikana leo

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Oktoba 20, 2021 inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Uamuzi huo unaotarajiwa kutolewa na Jaji Mustapha Siyani, uamuzi ambao utaweka picha ya mwelekeo wa kesi nyingine ndogo ndani ya kesi hiyo.

  > Kesi ya Mbowe yatupiliwa mbali

Kesi hiyo ndogo inahusiana na uhalali wa maelezo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Adamu Hassan Kasekwa, ambayo mawakili wa utetezi waliyapinga yasipokelewe kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Upande wa utetezi uliyapinga ukidai yametolewa nje ya muda wa kisheria na kwamba mshtakiwa huyo hakuyatoa kwa ridhaa yake bali kabla na wakati wa kuchukuliwa maelezo hayo alitishiwa na kuteswa.

Endapo mahakama itakubaliana na hoja za upande wa mashtaka, basi itayapokea maelezo hayo na kuwa kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

error: Content is protected !!