Kesi ya Mbowe yatupiliwa mbali

HomeKitaifa

Kesi ya Mbowe yatupiliwa mbali

Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi ya kikatiba ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, aliyekuwa akipinga namna alivyokamatwa, kuwekwa kizuizini na utaratibu uliotumika kumfunglia kesi ya ugaidi.

Mbowe alifungua kesi (kesi namba 21 ya 2021)  Julai 30, mwaka huu akilalamikia namna alivyotiwa mbaroni jijini Mwanza kuweka mahabusu ya polisi kwa siku tano bila kufikishwa mahakamani. Alidai kuwa alifikishwa mahakamani bila kuwajulisha mawakili wake au ndugu zake na kabla ya kujulishwa kwa maandishi kuhusu mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.

Uamuzi wa kuitupa kesi hiyo umetolewa leo  Jaji John Mgetta aliyesikilizaza pingamizi hilo la Serikali ambapo Mahakama imekataa hoja tatu za pingamizi la Serikali na kukubaliana na hoja moja ya pingamizi la Serikali kuwa Mbowe hakutumia njia nyingine zilizopo kutafuta haki anazodai kabla ya kufungua kesi ya kikatiba.

Kwa mantiki hiyo, kesi ya ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu itaendelea kusikilizwa.

error: Content is protected !!