Maofisa wa polisi kizimbani leo kesi ya Mbowe

HomeKitaifa

Maofisa wa polisi kizimbani leo kesi ya Mbowe

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Alhamis Septemba 16, 2021 itaendelea kupokea ushahidi wa jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mashahidi hao ni pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi, akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Wengine ni maofisa wa polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo vitengo vya makosa ya kimtandao, uchunguzi wa silaha na uchunguzi wa maandishi na wengine kutoka mikoani.

error: Content is protected !!